Wateja wengi wana nia ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi lakini hukumbwa na maswali mengi kabla ya kuanza. Katika makala hii, Masha Global Link tumekusanya maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQ) ili kukupa ufafanuzi wa haraka na sahihi kuhusu huduma zetu za uagizaji wa bidhaa.
1. Je, ninaweza kuagiza bidhaa bila kuwa na uzoefu wa awali?
Ndiyo. Masha Global Link tunawahudumia hata wateja wasio na uzoefu wowote wa uagizaji. Tunakuongoza hatua kwa hatua kuanzia kuchagua bidhaa hadi kuipokea Tanzania.
2. Ni aina gani za bidhaa naweza kuagiza kupitia Masha Global Link?
Unaweza kuagiza bidhaa mbalimbali ikiwemo:
Vifaa vya kielektroniki
Bidhaa za matumizi ya nyumbani
Vifaa vya biashara
Mitambo midogo na ya kati
Iwapo bidhaa haipo kwenye website, unaweza kutuma maombi kupitia Request Quotation page.
3. Je, ninawezaje kuwasilisha ombi la kuagiza bidhaa?
Unaweza:
Kuchagua bidhaa moja kwa moja kwenye website na kulipia
Kutuma request ya maelezo zaidi
Kutuma maombi ya bidhaa kupitia Request Quotation page
Kubofya kitufe cha WhatsApp kilichopo website kwa msaada wa haraka
4. Njia gani za malipo zinakubalika?
Tunatumia njia za malipo zilizo salama na rasmi. Mteja hupewa maelezo ya malipo baada ya makubaliano ya gharama.
5. Inachukua muda gani kupokea mzigo?
Muda wa kupokea mzigo hutegemea:
Aina ya bidhaa
Njia ya usafirishaji (bahari au anga)
Kwa kawaida:
Njia ya anga ni ya haraka zaidi
Njia ya baharini ni ya gharama nafuu
6. Je, mzigo wangu uko salama?
Ndiyo. Tunahakikisha mzigo unafuatiliwa kuanzia ulipoagizwa hadi unapofika Tanzania. Usalama wa mzigo na uaminifu ni kipaumbele chetu.
7. Vipi kama nahitaji msaada wa haraka?
Kwa msaada wa haraka:
Bofya kitufe cha WhatsApp kilichopo upande wa kulia chini mwa website
Wasiliana moja kwa moja na timu yetu kwa ushauri wa papo kwa papo
8. Kwa nini nichague Masha Global Link?
Uzoefu wa vitendo kwenye uagizaji
Huduma ya uwazi na ya kuaminika
Mawasiliano ya karibu na mteja
Mfumo rahisi wa kuagiza kupitia website
Hitimisho
Maswali haya yamelenga kukupa uelewa na kuondoa hofu yoyote kuhusu kuagiza bidhaa kupitia Masha Global Link. Tupo tayari kukuhudumia na kukuongoza kwenye safari yako ya biashara.
📞 Wasiliana Nasi: 0756 428 187 📍 Masha Global Link & MGL Store
Pamoja, tunaunganisha fursa na mafanikio.
Masha Global Link Connecting Opportunities, Building Trust.